"Baba yako alikuwa akisema ukweli, lakini inavyoonekana, hakufikiria kwamba ulikuwa mwaminifu wa kutosha kujua maelezo yote.
Pia alijua siri zote ambazo hazijazungumziwa. Ruegra alishangaa. Baba yake alikuwa ametaja siri hiyo mara nyingi, lakini hakuwahi kuwa na hamu ya kufichua.
"Nini mbaya, Jenerali? Unashangaa kwanini hakukuambia zaidi kuihusu?"
"Labda umri wangu mdogo na msukumo wangu ulinifanya msikilizaji mbaya."
"Afadhali niseme kwamba tabia yako ni hamu ya kuwa na mamlaka na utawala wa kijeshi."
"Mamlaka ni muhimu kudumisha utulivu na uimara." Akasisitiza Jenarali huyo, baada ya kusimama akiwa amekasirika.
"Una imani na utaratibu, ukiwa umeajiriwa kuhudumia mtu mmoja na kwa utulivu wa kabila moja." akajibu Wof.
Ruegra alianza kutembea kwa uwoga. Alikuwa tayari amepoteza uvumilivu wake, lakini alijua vizuri kuwa hakuna mateso au ulafi ambao ungefanya kazi kwa mtu ambaye alikuwa ameketi mbele yake. Tumaini lake la pekee lilikuwa kupata uaminifu wa mtu huyo.
Alianza kuwa mjanja na kudanganya:
"Unajua, kwa kweli ninamheshimu baba yangu. Wakati nilipokuwa mdogo ulikuwa ukisema kwamba ninafanana naye... Wakati huo, nilikuona kama bwana...."
"Nini inakufanya kufikiria kwamba nitafichua jinsi ya kupata ngozi hiyo? Usafi huo uliokuwa nao utotoni ulipotea haraka, Ruegra, na nia ya kujithibitisha ilichukuliwa na kiu ya mamlaka."
"Mimi si Aniki ambaye unamkumbuka wakati wa vita. Nitajua kuthibiti mamlaka kwa usawa. Baba yangu alifanya makosa kwa kukosa kuniambia kila kitu." "Jenerali alisema kwa hasira nyingi.
"Ikiwa ilibidi uje kwangu, inamaanisha kuwa haukustahili kuaminiwa na baba yako. Ni baba wa aina gani anayeficha maarifa kutoka kwa mwanawe? Kuna taabu katika ishara zake. Nani aliyebora kuliko yeye alikujua na mimi ni nani kufichua kila kitu kwako na kupuuza kabisa tathmini yake? Kama unavyoona siwezi fanya chochote lakini kuheshimu nia yake na kuheshimu kumbukumbu yake." Alisema Wof. Kisha alisimama na kusema kwaheri kwa mnyongaji wake.
Tukio hilo halingeondoka katika akili ya Jenarali, ambaye aliendelea kutazama angani akiwa na glasi mkononi kwenye usiku huo wa Bonobo uliokuwa joto.
Asubuhi iliyofuata, Ruegra alichunguza binafsi kazi ambayo ilikuwa imekamilishwa kubadilisha sehemu iliyoharibika ya chombo cha angani.
Mastigo alikuwa amefuatilia vizuri na mafundi wake walikuwa wamefanya kazi nzuri kama kawaida. Wakaondoka kwa wakati uliowekwa na kurejea nyumbani.
Siku zilikuwa zikipita na Ruegra alikuwa na haraka ya kurudi nyumbani. Aliogopa njama, ingawa kakaye, ambaye alikuwa akiongoza wakati hakuwepo, atampa Jenarali ripoti za kila mara kuhusu hali hiyo. Hapakuwa na kitu cha kuwa na wasi wasi nacho. Carimea ilikuwa mchanganyiko wa jamii. Makabila tofauti walikuwa wakipigania utawala dhidi ya Wa-aniki, lakini Wa-aniki walikuwa wamewaondoa idadi inayodhihirika ya wapinzani wakati wa utawala wao. Ilikuwa imeanzishwa na vikundi kadhaa vya mfumo tofauti wa jua, wengi wao walikuwa watalii, watafutaji wa bahati au wafungwa wa awali ambao walikuwa wakitafuta ardhi kuanzisha maisha yao upya. Sehemu ndogo tu kati yao walitoka kwenye sayari hiyo. Kwa kweli, watu wa sehemu hiyo walikuwa wametawaliwa kishenzi na kutengwa.
Njiani wakirudi, huku akiwa ameketi katika kiti cha kuthibiti chombo kwenye dashibodi, Ruegra alikuwa akifikiria kuhusu maneno ya Wof. Kwamba "Baba yangu alijua" iliendelea kusikika akilini mwake.
Kisha kwa ghafula, akafikiria nyakati zote baba yake angeondoka wakati wa msimu wa uwindaji na kabla ya vita vyote. Mahali alipenda kwenda ilikuwa kwa kweli ardhi ya Bonobo, haswa kwa Bahari ya Unyamavu.
Wakati fikra hizo zilikuwa zikitembea kwenye akili yake, alipata utambuzi wa kuangaza na kufikira:" Mbona sijafikiria kuhusu haya awali?" Kitu au mtu huku huenda alimpa taarifa zaidi kuhusu ngozi hiyo iliyo na siri.
Alihusisha uhisi wake na ripoti ya Mastigo kuhusu chombo cha angani cha kibiashara. Labda mtu alikuwa mbele yake.
Aliamuru kubadilisha njia mara moja. Walikuwa wanarejea huko Bonobo.
Mastigo, aliyekuwa ameshangaa baada ya kuwaona wakirudi, alikimbia kuelekea chombo hicho cha angani.
"Ninasalimu mtu ambaye hawezi kushindwa miongoni mwa watu wa Carimea. Jenerali, mbona umerudi?"
"Nimetafakari kuhusu kutua kwa chombo hicho cha angani, na imenishawishi kurudi na kushughulikia binafsi hali hiyo."
"Kwa mara nyingine, umefanya jambo la busara. Wataarifu wangu hawakurejea Bonobo. Kwa hivyo, niliamua kuzuru eneo hili mimi binafsi. Niligundua kuwa walikuwa wameondolewa na watu wasiojulikana."
Ruegra alikuwa akitumaini kuwa Gavana wake hajaharibu uwezekano wote wa kupata taarifa kwa kuwa alijua njia zake.
"Hakuna kilichoachwa huko." akaripoti Mastigo mara moja, ambaye alikuwa akionekana kuridhika kama mtoto ambaye alitesa mawindo yake madogo.
Ruegra alijizuia kumshambulia msemaji wake na kumwuliza mahali wafanyakazi wake walikuwa wameenda.
Mastigo alichukua pumzi mzito, akifahamu kuwa haitakuwa Habari njema.
"Hatukuweza kuipata. Lazima wamekimbia."
"Sio tu uliharibu ushahidi wote, lakini pia uliwaacha wafanyakazi kutoroka! Ulikuwa huna ujuzi wewe! Nipeleke huko!"
Kisha, baada ya kufikiria tena alitambua kuwa haitakuwa wazo nzuri kumruhusu Mastigo kufahamu kuhusu mipango yake.
"Niandalie wafanyakazi. Nitaondoka kesho bila wewe."
Sura ya Pili
Upanga wa jiwe ulikuwa ukining'inia juu ya vichwa vyao.
"Tujiandae? Huenda tusikaribishwe tukapowasili! "alishangaa Oalif, ambaye ni mwerevu zaidi kwenye kundi hilo.
Wafanyikazi walijumuisha wanachama wanne kutoka sayari ambazo zilikuwa zikipambana dhidi ya utawala wa Carimea. Walichaguliwa kwa sababu ya historia yao ya matumizi na pia uwezo wao wa mwili na akili. Kwa pamoja wangeunda timu ambayo ingeweza kufanya kazi yoyote, nyingi na kimkakati. Wajibu wao ulikuwa kuhakikisha amani na sio tu hatua za kijeshi, lakini pia shughuli zinazohusiana na ujasusi na uratibu kati ya watu tofauti.
Baraza la Muungano wa Sayari Nne lilikuwa limewateua kuwa "Tetramiri", ambayo ilimaanisha kwamba wanaweza kufaidika na Serikali kutoka kwa mamlaka maalum na kazi hadi kukamilika kwa utume wao.
Meli ndogo cha angani cha kibiashara kilikuwa kikivuka miviringo mikubwa za kijivu za Bonobo na kilikuwa kikiendelea kuelekea Bahari ya Ukimya.
Aina hiyo ya chombo cha angani ilitengenezwa kwa minajili ya usafirishaji wa bidhaa. Iliumbwa kama mabomba sambamba yaliyo na kingo zilizobutu mbele ili kutoa mwendo mzuri angani. Juu ya hayo, ilikuwa wameweka mabawa madogo, yanayoweza kutolewa ambayo yalitumika wakati wa kuvuka anga. Nyuma, kulikuwa na mlango mkubwa wa kushikilia ambao ungefunguliwa katika sehemu tatu kama taji ya maua na ilitumika wakati wa kupakia na kupakua. Vyombo hivyo vya angani vilikuwa kubwa na mwendo wa polepole. Vingeondoka na kutua sambamba na ardhi bila hata kuacha nafasi yoyote ya badiliko la mwelekeo wa mapigo, kama vyombo vingine vile vya angani.
"Jitangaze." sauti ya metali ilitoka redioni.
"Sisi ni wafanyabiashara, bwana." alijibu Oalif.
"Tunaweza kuona. Lakini ni nani na ni nini mmebeba? Una leseni? "
"Settimo kutoka Oria, bwana."
"Nambari ya leseni, sasa!" alisisitiza mlinzi.
"34876."
"Wewe haumo katika orodha yetu. Badilisha njia mara moja. Huna ruhusa yoyote ya kutua katika eneo hili. "
"Mawimbi ni dhaifu, bwana. Sikusikii. Leseni namba 34876. "alisema Oalif kwa mara ya pili, akijifanya hasikii kile mlinzi alikuwa anasema.
"Ruhusa ya kutua imekataliwa!"
"Hatuwezi kunakili wewe, bwana." alisisitiza mtu huyo wa Bonobo kisha akawaambia wafanyakazi wake akisema: "Tuko ndani, jamani! Tunavuka ukungu katika Bahari ya Ukimya! "
Oalif